News and Events

LUGHA YA KICHINA YAWAPELEKA NJE YA NCHI ZAIDI YA WANAFUNZI 15 KUTOKA MUM.


Zaidi ya Wanafunzi 15 kutoka Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro(MUM) wamepata nafasi ya Ufadhili wa masomo Nchini China baada ya kufanya vizuri katika mafunzo ya Lugha ya Kichina inayofundishwa Chuoni hapo.


Akizungumza mara baada ya hafla ya utoaji tuzo ya Mwaka ya Balozi wa China inayotolewa kwa

wanafunzi  kutoka Vyuo na shule zinazofundisha Lugha hiyo, Mkufunzi wa Lugha ya Kichina kutoka MUM Tariki Kiangi amesema idadi hiyo ya wanafunzi waliopata fursa ya masomo Nchini China ni sehemu ya wanafunzi wengi mahiri katika kuzungumza na kuandika Lugha hiyo Chuoni hapo.

Amesema wanafunzi wengi wameendelea kuonesha mwamko wa kujifunza Lugha ya Kichina kutokana na fursa mbalimbali za ajira zinazotokana na kujifunza Lugha hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika tarehe 14 Novemba, 2025 katika ofisi za Ubalozi wa China Jijini Da es Salaam, Balozi wa China hapa Nchini Ming Cheng Jian amesema China itaendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo uwekezaji ambao unatoa fursa za moja kwa moja kwa wanafunzi wanaojifunza Lugha ya Kichina.