MUM YASHIRIKI SEMINA YA PILI YA TANZIE
Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kimeshiriki katika Semina Maalum ya kuwajengea Uwezo wakufunzi yenye lengo la uboreshaji wa Elimu ya Tanzania katika ngazi ya Kimataifa.
Semina hiyo ya siku tatu ni ya pili ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kwa wakufunzi kutoka Vyuo Vikuu vya Tanzania katika Mkakati wa kupileka elimu ya Tanzania kimataifa ujulikanao kwa lugha ya Kigeni kama The Tanzania Internationalisation Strategies for Higher Education (TANZIE) safari hii ikifanyika katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela African Institution of Science and Technology (NM-AIST) kilichopo Mkoani Arusha kuanzia June 15 hadi 17, 2026.
Semina hiyo inavikutanisha Vyuo Vikuu vya ndani ikiwa ni Pamoja na Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM), Catholic University of Health and Allied Sciences (CUHAS) na NM-AIST Saarland University, Tume ya Vyuo Vikuu Nchini Pamoja na European Foundation for Management Development (EFMD) Global amba oni wadau wa Kielimu Kutoka Nje ya Tanzania.
Katika Siku ya 1, washiriki wamehudhuria vikao vilivyolenga muhtasari wa "Ukimataifa wa Ndani ya Nchi" (IaH), huduma za usaidizi kwa wanafunzi wa kimataifa wanaoingia kupitia Vituo vya Mapokezi (Welcome Centers), na mifumo ya kusaidia wanafunzi wanaotoka nje kupitia Vituo vya Huduma za GoOut.
Vikao hivyo viliendeshwa na Bettina Jochum kutoka Chuo Kikuu cha Saarland (USAAR), ambaye alisisitiza jukumu muhimu la uongozi wa taasisi katika kuendesha ajenda za ukimataifa zenye mafanikio.